Jumapili , 2nd Oct , 2022

Kutokana na upotevu wa hekta 372,000 za misitu kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu hali iliyopelekea wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kuja na kampeni ya upandaji miti nchi nzima na kufanya doria kwenye hifadhi zote ili kuondoa shughuli za binadamu zinazopelekea ukataji miti.

Kamishna Msaidizi  wa Wakala wa huduma za Misitu nchini Dokta Masota Abed

Hayo yamesemwa na Kamishna Msaidizi  wa Wakala wa huduma za Misitu nchini Dokta Masota Abed, mara baada ya zoezi la upandaji wa miti mkoani Geita na kusema kuwa shughuli za kibinadamu zimechangia kwa kiasi kikubwa kumaliza misitu nchini.

"Kwa Tanzania takwimu za 2015 zinaonesha kuwa nchi inapoteza kiasi cha hekta 372,000/ kwa mwaka, sasa hii misitu inapotea kwa njia gani, imekuwa kwamba aidha shughuli za kibinadamu ambazo kama kilimo, uchimbaji madini na suala la nishati, nishati sana sana ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa", amesema Abed

Katibu Tawala wa mkoa wa Geita Professa Godius Kahyarara, amewashauri wakala wa huduma za misitu kuandaa kampeni ya kupunguza ukataji miti kuliko uoandaji miti.