Ijumaa , 1st Apr , 2016

Viongozi wa shirikisho la Vyama vya waajiri katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamewataka viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuoananisha sera za kitaifa za masuala ya kazi pamoja na sheria za kazi ili kurahisisha ufanyaji kazi nchi wa

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya waajiri katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,Dkt. Aggrey Mlimuka

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Arusha Katibu wa shirikisho hilo Dkt. Aggrey Mlimuka amesema kuwa iwapo nchi hizi zikiainisha sera hizo pamoja na sheria zirahishsa vijana kutoka nchi moja hadi nyingine kutafuta ajira kwa urahisi zaidi.

Dkt. Mlimuka amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya Uongozi wa katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki dkt. Richard Sezibera ameweza kuleta mafanikio makubwa ikiwemo kuondoa malipo ya vibali vya waajiri kwa nchi tatu.

Aidha Dkt. Mlimuka ameongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo wanaiomba jumuiya ya Afrika mashariki kuoanisha sera hizo na sheria ambapo itakua ni mafanikio makubwa zaidi kwa jamuiya hiyo katika kukuza soko la Ajira.

Aidha ametumia fursa hiyo kumpongeza rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo na kusema mategemeo yao kuwa kauli yake mbiu ya Hapa kazi tu itadhihirika katika jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Vyama vya Waajiri katika nchi za Afrika Mshariki, Rosemary Ssenaburi amesema shirikisho la vyama vya waajiri katika nchi za jumuiya ya afrika mashariki iwapo wananchi hawatakua na uhuru wa kutoka nchi moja kwenda nyingine hawataweza kupiga hatua.

Sauti ya Katibu wa Shirikisho la Vyama vya waajiri katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,Dkt. Aggrey Mlimuka kuhusu ombi lao kwa viongozi wa Afrika Mashariki