Jumatatu , 27th Sep , 2021

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga George Kyando ameikaribisha timu ya East Africa TV na East Africa Radio ambayo ipo wilayani humo kwaajili ya kugawa taulo za kike kwa wanafunzi kupitia kampeni ya Namthamini 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga George Kyando

''Karibuni sana mkoa wetu wa Shinyanga kwa ujumla hali ya ulinzi na usalama ya mkoa ni njema na natumaini mmeingia salama na mtatoka salama'', ameeleza RPC George Kyando.

Aidha RPC Kyando ameongeza kuwa ndani ya mkoa huo kuna ukatili dhidi ya watoto wa kike na makosa ya kijinai dhidi ya watoto wa kike na hii inasabishwa sana na ndoa na mimba za utotoni''.

Wafanyakazi wa East Africa TV na East Africa Radio wakiwa na mkuu wa Wilaya ya Shinya Jasinta Mboneko (katikati)

Timu ya Namthamini ikiongozwa na watangazaji Samson Charles pamoja na Najma Paul ipo mkoani Shinyanga kwaajili ya zoezi la ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za sekondari katika wilaya za Shinyanga na Kishapu.