Jumanne , 28th Jan , 2020

Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya, amesema kuwa atahakikisha anasimamia haki na misingi ya Bunge kwa maslahi ya wananchi na kutoa rai kwa Spika wa Bunge Job Ndugai, kuhakisha unakuwepo ushirikiano kwa ajili ya kuitendea nchi haki na Bunge kiujumla.

Mbunge wa Bunda Mjini na Mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani, Esther Bulaya.

Akizungumza leo Januari 28, 2020 na EATV&EA Radio Digital, mara baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumtangaza kuwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani, katika Mkutano wa 18, kikao cha Kwanza, jijini Dodoma.

"Nimepokea kwa furaha lakini najua majukumu ya hiyo nafasi, kikubwa ni ushirikiano wa Wabunge wa pande zote mbili kwa maslahi ya wananchi, tunatakiwa tufuate kanuni na kuzitafsri inavyotakiwa, na naahidi kuhakikisha natetea na kupigania haki bila chembe ya uoga, maslahi ya kambi rasmi ya upinzani na niko tayari ku sacrifice kwa sababu maoni mengi ya kambi rasmi yanagusa maoni ya wananchi" amesema Ester Bulaya.