Jumanne , 18th Oct , 2016

Ethiopia imepiga marufuku upatikanaji wa vyombo vya habari vya upinzani vyenye makao yake nje ya nchi na kuwazuia mabalozi kusafiri katika hatua yake mpya ya hali ya hatari.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.

Siku nane zilizopita, serikali ya nchi hiyo ilitangaza hali ya hatari kwa kipindi cha miezi sita kufuatia maandamano ya kuipinga ambayo hadi sasa yamewaua mamia ya watu nchini humo.

Moja ya hatua hizo mpya zilizochapishwa katika vyombo vya habari hapo jana ni pamoja na marufuku ya kubeba silaha katika eneo lenye ukubwa wa 50 katika mpaka wa nchi hiyo.

Aidha mabalozi wa nje wamezuiwa kusafiri zaidi ya kilomita 40 nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa kwa ajili ya usalama wao, huku vyama vya upinzani vikipigwa marufuku kutotoa taarifa kupitia vyombo vya habari, ambazo zinachochea vurugu.