Jumanne , 18th Jun , 2019

Mkazi mmoja wa Mtaa wa Kashaulili Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi, Mbahige Nsanyi Chiha, amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuwatibu baadhi ya wagonjwa waliovunjika mifupa kwa tiba za kienyeji na wagonjwa hao wakipona.

Awali baadhi ya wagonjwa hao walishindwa kupata huduma ya kutibiwa sehemu walizovunjika katika Hospitali ya Mkoa wa Katavi,na kulazimika kwenda kwenye Hospitali za Rufaa huku wenyewe wakiwa hawana gharama za kumudu matibabu hayo.

Akizungumza na www.eatv.tv, Chiha amedai kuwa yeye ni mganga wa tiba  asili na amekuwa akitoa matibabu kwa wagonjwa mbalimbali waliovunjika mifupa kwa njia ya asili.

"Hii huduma yangu inatambulika kisheria hasa kwa wagonjwa ambao wanashindwa kugharamia matibabu yao kuvunjika mguu, mimi ninachokifanya nampeleka kwenye eneo langu la kumtibia halafu namwambia anyooshe mguu ambao ni mzima kisha nachukua kivuli cha mchanga wa mguu ambao haujavunjika kisha naanza kumtibia", amesema Mganga Chiha.

Miongoni mwa wagonjwa walipatiwa huduma na bwana Chiha ni Joseph Peter pamoja na Konsolata Kasimele ambao ni wakazi wa Manispa ya Mpanda waliwahi kutibiwa.

Mtazame hapa chini akionesha matibabu yake