Alhamisi , 2nd Apr , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, ameagiza kusimamishwa kazi kwa Afisa Ugavi wa Wilaya hiyo Sabian Wambura, baada ya kuchelewesha ujenzi wa kituo cha afya cha Kwatito na kuiagiza Halmashauri kukamilisha ujenzi huo ndani ya siku 14.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Kwa mujibu wa DC Sabaya ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha afya umechelewa, kwani fedha za ujenzi huo ziliwasilishwa tangu Agosti 2019, lakini hadi sasa ujenzi huo bado haujakamilika.

"Inawezekanaje fedha zinaletwa mwezi wa 8, Milioni 30 ziko tu benki, fedha za umma si za kwako wewe Wambura wala Mkurugenzi na zimeletwa ili kusaidia hawa wananchi wa maisha ya kawaida kabisa, nataka ndani ya siku 14 hili jengo liwe limekwisha, TAKUKURU anzeni na huyu, Mkurugenzi huyu achukuliwe hatua asimamishwe" amesema DC Sabaya.