Jumatano , 9th Oct , 2019

Wafanyabiashara, vijana na wananchi, wametakiwa kuchangamkia fursa kutoka kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance, ili kusaidia kuweka kinga dhidi ya majanga yote yanayohusiana na pesa pamoja na hasara za kiuchumi katika uzalishaji.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Bima ya Jubilee

Wito huo umetolewa leo Oktoba 9, 2019, jijini Dar es salaam na Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Wateja wa Rejareja kutoka Jubilee Insurance Bw. Abdulrauf Suleiman, wakati wa mahojiano maalumu katika muendelezo wa kampeni ya Kibiashara Zaidi inayoendeswa na vituo vya East Africa Television na East Africa Radio, ambapo ameeleza kuwa wanatoa bima katika maeneo mbalimbali ikiwemo maisha, Magari, Afya na Kilimo.

“Mfano bima ya magari ambayo ni kinga anayopatiwa mteja kusaidia kuokoa matumizi ya fedha endapo chombo hicho cha usafiri kitapata ajali ya kugongwa au moto ambazo zimegawanyika katika makundi mawili bima kubwa na ndogo”.

Amesema kuwa kampuni hiyo ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka 30, imefanikiwa kutwaa tuzo nne ambazo zinadhihirisha uwezo wake katika utoaji huduma katika jamii, huku akiwataka wateja wafahamu umuhimu mkubwa wa kuweka kinga katika maeneo tajwa, ili kusaidia kuokoa hasara katika uzalishaji na uendelezaji wa shughuli za kiuchumi.

Amesema kuwa ni vyema wateja wakafahanu umuhimu mkubwa wa kuweka kinga, katika maeneo tajwa ili kusaidia kuokoa hasara katika uzalishaji na uendelezaji wa shughuli za kiuchumi.

Aidha amesisitiza uwepo wa fursa ya uwekezaji katika bima, ikiwa wao wamejikita katika utoaji wa huduma zaidi ya 30, hivyo kutoa nafasi za ajira kwa vijana kuweza kufungua ofisi ndogo ya bima kama wakala.

'Mpaka sasa mafanikio makubwa yamekuwepo   kutokana na utolewaji wa elimu kwa wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali katika jamii kuhusu kuweka kinga katika vitega uchumi vyao', ameeeleza.

Amemaliza kwa kutaja kuwa fursa ya uwekezaji katika bima ni kubwa ambapo mpaka sasa wao wamejikita katika utoaji wa huduma zaidi ya 30, hivyo kutoa nafasi za ajira kwa vijana kuweza kufungua ofisi ndogo ya bima kama wakala.