
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa Maigwa,
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Simon Marwa Maigwa, amesema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 30,2020, na kwamba mara baada ya kufanya tukio hilo alikimbilia kusikojulikana na kumtaka ajisalimishe kokote alipo kwani mkono wa sheria ni mrefu utamfikia.
Aidha Kamanda Maigwa, amesema kuwa katika kuelekea kipindi hiki cha kilimo ni vyema migogoro yote ya mashamba ipelekwe kwenye ngazi za sheria na siyo kujichukulia sheria mkononi.