Jumamosi , 11th Jun , 2022

Watanzania wamehamasishwa kuanza kutumia nishati ya gesi asilia kwenye magari yao, kutokana na unafuu wa gharama yake ukilinganisha na matumizi ya magari yanayotumia mfumo ya mafuta ya petrol au dizeli.

Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba

Wito huu umetolewa leo Juni 11, 2022 na Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati mhandisi Felchesmi Mramba akichangia mada katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao ‘zoom’, huku akisistiza kuwa tayari wataalamu nchini wathibitisha kuwa kuna uwezekano wa gari ya aina yoyote kubadilishwa mfumo kutoka matumizi ya mafuta na kuanza kutumia gesi.

"Gari ya aina yoyote inaweza kubadilishwa mfumo kutoka matumizi ya mafuta na kutumia gesi, na bei yake ni nafuu zaidi ukilinganisha na matumizi ya mafuta, unaweza kuokoa zaidi ya nusu ya gharama inayotumika kwenye mafuta." Amesema Katibu mkuu Wizara ya Nishati mhandisi Felchesmi Mramba 

Aidha Mhandisi Mramba amebainisha kuwa, uwepo wa gesi umesaidia kuondoa mgao wa umeme nchini kwani asilimia 62 ya umeme wote unaozalishwa nchini unatokana na gesi asilia.

Awali akitoa historia ya upatikanaji wa gesi asilia nchini Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati amebainisha kuwa mwaka 1974 wataalam waliokuwa wakitafuta mafuta, walikutana na gesi asilia badala ya mafuta ardhini.