Alhamisi , 2nd Jul , 2015

Serikali imewataka wananchi wa mkoa wa Mtwara kuwa na subira juu ya kunufaika na rasilimali ya gesi, kwani faida yeke kwa wananchi hao itaanza kuonekana baada ya miaka 10 ijayo.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda

Hayo yamezungumzwa jana mkoani humo na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, wakati akihutubia katika sherehe za kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya serikali za mitaa zilizofanyika katika viwanja vya mashujaa.

Pinda amesema kuna haja ya kuiboresha bandari ya Mtwara kwasababu ndiyo itakayotumika kusafirishia sehemu ya gesi itakayo zalishwa kutoka katika kina kirefu baharini .

Aidha Pinda ameongeza kuwa gesi hiyo ambayo matumizi yake yanatarajiwa kuanza ndani ya miaka 10, lazima ikitolewa huko ifike mjini Mtwara ambako ndiko kitakuwa kituo cha kuisafirisha.