Alhamisi , 5th Feb , 2026

Mtoto mmoja kati ya watatu waliokuwa wakioga kwenye mto Simiyu  uliopo  kata ya Zanzui wilayani Maswa mkoani Simiyu ameuwawa na mamba huku baadhi ya viungo vya mwili wake vikiwa vimeliwa.

Mtoto mmoja kati ya watatu waliokuwa wakioga kwenye mto Simiyu  uliopo  kata ya Zanzui wilayani Maswa mkoani Simiyu ameuwawa na mamba huku baadhi ya viungo vya mwili wake vikiwa vimeliwa.

Mtoto huyo  ametambulika kwa jina la Paulo Petro Bunga  mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikuwa wa pili kutoka kwenye maji lakini mamba akampiga na mkia na kumzamisha kwenye maji huku wenzake wakishuhudia tukio hilo.

Mmoja wa watoto walionusurika  ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Zanzui  iliyopo wilayani humo Emmanuel Robert anasema awali alihisi kitu akawashtua wenzake wawili huku akiwa tayari nje ya maji.

"Niliwashtua wenzangu tukoke nje Paul alikuwa wapili kutoka nje mamba akampiga na mkia akamzamisha ndani ya maji nilichanganyikiwa badae nikakimbia kwenda kwao kuwaambia" anasimulia kwa uchungu
Robert