Alhamisi , 31st Mar , 2016

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imebaini kuongezeka kwa gharama za mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka shilingi bilioni 214 hadi shilingi bilioni 300.

Muonekano wa Daraja la Kigamboni

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam baada ya kukagua hatua za mwisho za ujenzi huo Mwenyekiti wa kamati hiyo Norman Sigalla amesema mkataba uliotiwa saini ulikua unaelekeza malipo yalipwe kwa fedha za kigeni na zingine za ndani.

Prof. Sigalla amesema kuwa wakati daraja hilo likianza kujengwa dola moja ilikuwa ni sawa na shilingi 1500, wakati hivi sasa dola mija ni zaidi ya shilingi 2100.

Kwa upande wake meneja wa mradi huo Mhandisi Karim Mattaka amesema ni kweli gharama za awali zilizotozwa kwa thamani ya dola ilivyokuwa ni sh. 1500 huku zaidi ya asilimia 88 ya fedha hizo tayari zikiwa zimeshalipwa.

Aidha Mhandisi Mattaka ameongeza kwa asilimia 25 ya gharama za ujenzi huo zimelipwa kwa fedha za Kitanzania na asilimia 75 zililipwa kwa fedha za Kigeni.