Jumatano , 4th Nov , 2015

Mgogoro wa kisiasa unaondelea kisiwani Zanzibar umeanza kuleta madhara yake baada ya bei za vyakula muhimu na vitoweo kupanda bei kwa asilimia kubwa na kuwaweka wazanzibari katika wakati mgumu.

Mfanyabiashara wa Mbogamb oga visiwani Zanzibar akielezea hali ya biashara viwasini humo

Bei za vyakula muhimu kama nyama ya Ng'ombe na Mbuzi kupanda kwa kilo moja kufika hadi 12,000 kutoka 8000, huku bei za viazi vikiuzwa kilo 2000, badala ya 800, vitunuguu karoti na matunda mengine yakipanda bei mara mbili zaidi huku bei za samaki nazo zikiendelea kuwa tishio ambapo samaki moja mkubwa alikuwa akiuzwa 16,500 badala ya 6500.

Baadhi ya wafanyabishara wa vyakula na kitoweo wakiongea visiwani humo wamesema hali hiyo inatokana na kuwa, kwa hivi sasa hakuna chakula cha aina yeyote kinachingia Zanzibar kutoka bara ambapo ndipo soko kubwa la mahitaji ya visiwa hivyo.

Naye moja ya wananchi ambaye alikuwa akitafuta mahitaji yake katika soko kuu la Zanzibar Abubakar Pandu amesema wanaumia na hali hiyo hivyo njia pekee ni wahusika wamalize na wao wanalazimka kununua kwa kuwa hawana sehemu nyengine ya kutafuta afueni