Ijumaa , 14th Oct , 2016

Halmashauri 7 kati ya 179 ambazo Mwenge wa Uhuru umemulika mwaka huu 2016 zimebainika kutumia vibaya fedha zinazotengwa asilimia 5% kwa ajili ya vijana.

Waziri, Jenista Mhagama

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama katika maelezo yake kuhusu mbio za Mwenge mwaka huu mkoani Simiyu

“Halmashauri 7 nchini zimebainika kutumia vibaya fedha za vijana ambazo zimetengwa kuwasaidia na nataka niseme hapa kwamba serikali inamalizia uchunguzi baada ya hapo wote waliohusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria” Amesema Mhagama

Mhagama ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kote nchini kuendelea kuchapa kazi kwani serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili yao na inathamini sana mchango wao katika jitihada za ujenzi wa taifa.

Aidha Waziri Mhagama amesema viongozi wote ambao hawataki kushirikiana na vijana katika mikoa yao na kutambua michango yao watachukuliwa hatua.

Mwenge wa Uhuru umemaliza shughuli zake mkoani Simiyu ambapo umezindua miradi ya maendeleo1,387 yenye thamani ya shilingi bilioni 498.5