Jumapili , 14th Mar , 2021

Halmashauri zilizokopeshwa fedha za kupanga, kupima na kumilikisha ardhi mkoani Iringa, zimepewa siku kumi na mbili na Kamati ya Ardhi Maliasili na Utalii  kuhakikisha zinarejesha fedha hizo ili kusaidia halmashauri nyingine ambazo hazijakopeshwa, kupima maeneo yao.

Mkuu wa mkoa wa  Iringa Ally Hapi

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Aloyce kwezi baada ya  kutembelea na kukagua mradi wa kupanga na kupima ardhi wa Igumbilo, uliotekelezwa na Manispaa ya Iringa kwa kutumia fedha za mradi walizokopeshwa na Wizara ya Ardhi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa  Iringa Ally Hapi amesisitiza kuwa ni lazima wakurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya hizo watambue wana wajibu wa kulipa fedha hizo.

''Mimi nadhani hakuna haja ya wakurugenzi kujitetea, hili liko wazi pesa ya kukopa inatakiwa kurejeshwa mara moja kwa utaratibu uliopangwa'', amesema.

Katika mikopo hiyo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, ilikopeshwa na Wizara ya Ardhi shilingi millioni 418, ambapo mpaka sasa wamerejesha milioni 100 pekee.