Jumanne , 18th Dec , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi ameonesha kushangazwa na madai ya kujikuta amelala kwenye makaburi mkoani Iringa, kitendo ambacho kinahusishwa na imani za kishirikina.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Hapi ameandika ujumbe ulioashiria kuwa analichukulia tukio hilo ni la mzaha ambapo aliambatananisha na picha yenye maneno yanayodai kufanyiwa kitendo hicho.

"Du, nimekumbuka hekaya na ndoto za abunuwasi" aliandika Hapi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Duuuh...Nimekumbuka hekaya na ndoto za abunuwasi.

A post shared by Ally S. Hapi (@ally_hapi) on

Aidha katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameamuru mtumiaji huyo wa mitandao ya Kijamii Hilda Newton kwena kujisalimisha kwa Mkuu wa Polisi Iringa kwa ajili ya kutoa maelezo kabla ya disemba 21 mwaka huu.

Kupitia ukurasa wa twitter wa mtu ambaye alisomeka kwa jina la Hilda Newton, aliandika,"Naambiwa mwezi mmoja uliopita, alikuwa amelala nyumbani kwake ilipofika alfajiri alijikuta amelala makaburini".

Mkuu huyo wa Mkoa kwa sasa yuko likizo ya mwezi mmoja Jijini Dar es salaam, ambapo majukumu yake ameyakaimisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela.

Mara kwa mara Hapi amekuwa akiingia kwenye mnyukano wa maneno na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Peter Msigwa pamoja na Meya wa Manispaa hiyo Allex Kimbe.