"Hatuwezi ku-copy wazungu, tutaua watu" - Ndugai

Jumanne , 31st Mar , 2020

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kama nchi haiwezi kuchukua tahadhari kama zilivyochukuliwa na Mataifa mengine duniani ya kupambana na Virusi vya Corona kwa kuwa watu wengi nchini maisha yao ni ya kubangaiza siku kwa siku.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai

Hayo ameyabainisha leo Machi 31, 2020, Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Mkutano wa 19.

"Hatuwezi kuchukua measure za wazungu na kuzi copy na ku- paste hapa kwetu kama zilivyo, tutaua watu wetu, lazima tuangalie maisha yetu ya Kitanzania na kujaribu kuchukua hatua kufuatana na mazingira yetu" amesema Spika Ndugai.

Aidha wakichangia hoja zao bungeni wabunge wa CHADEMA Halima Mdee na Peter Msigwa, wameishauri Serikali kuja na taarifa zote zinazohusu mwenendo wa ugonjwa wa Virusi vya Corona hapa nchini na kuangalia ni kwa namna gani kwa pamoja wataweza kukabiliana na athari ikiwemo uchumi pindi ugonjwa huo utakaposambaa zaidi.