Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Hizi ndio sababu za Lissu kutibiwa Nairobi

Ijumaa , 8th Sep , 2017

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, ametolea ufafanuzi suala la matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Antiphas Lissu aliyepelekwa Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi.

Akitoa taarifa hiyo mara baada ya sala ya kuliombea bunge asubuhi ya leo ili kuanza vikao, Spika Ndugai amesema utaratibu wa matibabu kwa mbunge yeyote ulikuwa umeshafuatwa lakini familia iliamua yenyewe kumpeleka Nairobi, na siyo kama walishindwa kumpeleka nchini India.

"Baada ya bunge kupata taarifa kuhusu tatizo hilo, sisi bunge tulikuwa tumeshaagiza ndege tayari ilikuwa uwanjani, hapa Dodoma kwa ajili ya kumpeleka Hospitali ya Muhimbili ambapo ndiyo utaratibu wa kibunge, na kama kuna rufaa ya nje ya nchi utaratibu wetu ni kwamba serikali yetu ina mkataba na hospitali ya Apolo kule India, na ndiyo 'channel' ya sisi wote. Lakini kwa nini mwenzetu alipelekwa Nairobi, ni kwa sababu familia iliomba na Mh. Mbowe alieleza na mimi nilinukuu kwa niaba yake, walisema siyo kama wana mashaka na umahiri wa madaktari wetu, lakini wangejisikia faraja kwa wao wenyewe kuachagua kumpeleka kutibiwa Nairobi", alisema Spika Ndugai.

Spika Ndugai aliendelea kusema kwamba tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu ni la kwanza tangu historia ya bunge kuhamia Dodoma kwa miaka mingi, na kulivitaka vyombo vya dola kushughulikia tatizo hilo, huku akiwaomba wananchi kuwa watulivu kwani hali yake inatia moyo.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu