Ijumaa , 5th Feb , 2021

Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini kupitia CCM, Emmanuel Mwakasaka, amehoji msimamo wa serikali kwa hospitali zinatowatoza fedha akina mama waliojifungua kwa njia ya kawaida na wanaoshindwa kulipa basi huzuiliwa kutoka hospitalini hapo.

Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka

Mwakasaka ametoa kauli hiyo hii leo Februari 5, 2021, Bungeni Dodoma, kwenye kikao cha Nne, mkutano wa Pili wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akiitaji hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete kuwa bado inaendelea kutoza fedha zinazoanzia kiasi cha shilingi 30,000 hadi shilingi 50,000 kwa akina mama hao.

"Hospitali ya Kitete Tabora bado inatoza fedha na ushahidi upo kwa akina mama waliojifungua kwa njia ya kawaida na wanaoshindwa kutoa hizo fedha huwa wanazuiliwa, je serikali ina msimamo gani kwa wale akina mama ambao huwa wanazuiliwa kutoka na watoto wao wachanga hadi walipe hizo fedha ambazo ni za kujifungulia?", amesema Mbunge Mwakasaka

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema kuwa msimamo wa serikali ni kwamba waganga wakuu wa mikoa na wilaya wahakikishe wanasimamia sera ya akina mama wanaoifungua kwa njia ya kawaida na wanajifungua bure na kuahidi kwamba ataongozana na mbunge hadi kwenye hospitali hiyo ili wakapige mahesabu na kuja na ufumbuzi