Jumapili , 28th Jun , 2020

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde, amesema jumla ya watahimiwa 85,546 ndio waliosajiliwa kufanya mitihani ya kidato cha sita na ualimu inayotarajiwa kuanza nchi nzima hapo kesho Jumatatu Juni 29, 2020.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde

Msonde amesema maandalizi yote yameshakamilika na kupitia mtihani huo watahiniwa hao ndio watakuwa wanapimwa uelewa wao katika masomo waliyokuwa wakisoma.

Aidha baraza pia limezitaka kamati za mikoa za kusimamia mitihani kuhakikisha wanasimamia mitihani hiyo na kusitokee udanganyifu wowote kwa watahiniwa.