
Bendera ya CHAUMMA
CHAUMMA ambayo katika Uchaguzi wa mwaka 2015 ilikuwa na wagombea wa Ubunge 23, ambapo wanaume walikuwa 14 na wanawake 9 huku nafasi za Udiwani walisimamisha wagombea 27 nchi nzima, wanaume 24 na wanawake watatu.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, Naibu Katibu Mkuu Bara wa CHAUMMA, Eugene Kabendera, amesema kuwa kufikia Agosti 25 watakuwa na idadi kamili na itafahamika kama watasimamisha wagombea kila Jimbo na Kata au wataungana na vyama vingine.
"Bado tupo kwenye mazungumzo ya namna tutakavyoshirikiana na vyama vingine, itafahamika muda si mrefu kama tutasimamisha wagombea wetu kila mahali au tutaungana na wenzetu katika baadhi ya maeneo", amesema Kabendera.
Wakati wagombea hao wakisubiri kupitishwa na chama hicho tayari Mwenyekiti wa CHAUMA Hashim Rungwe, amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo Dodoma.