Jumamosi , 12th Sep , 2015

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mh. Idd Azzan amesema kuwa endapo atapata ridhaa ya wananchi kwa kuwawakilisha kwa mara nyingine atasaidia kuboresha sekta ya afya na kutatua tatizo la Ajira kwa Vijana.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mh. Idd Azzan

Akizungumza na East Africa Radio leo wakati akielezea Ufunguzi wa Kampeni wa chama hicho katika jimbo hilo Mh. Idd Azzan amesema kuwa ataanza kuishughulikia Hosptali ya Mwananyamala ambaoyo inaonekana imediwa na idadi ya Wagonjwa lakini ataongeza ajira kwa vijana kwa ni tatizo pia linalowakabili wakazi wa eneo hilo.

Adha Mh. Azzan ameongeza kuwa suala lingine atakalolipa kipaumbele ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ya jimbo hilo hasa barabara pamoja na mifereji ya maji taka laini pia atahakikisha wakazi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama.

Katika hatua nyingine mbunge huyo anayemaliza muda wake katika jimbo hilo amesema ataendesha kampeni za kistaarabu bila kuwashambuliwa wagombea wa vyama vingine na kuahidi pia hata atakapopata nafasi kati ya watu atakaofanya nao kazi kwa ukaribu ni pamoja na washidani wake kwa sasa.