Jumanne , 1st Sep , 2015

Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wameendelea na kampeni za kuwania Urais kwa mgombea wa chama hicho Mh. Edward Lowassa katika mkoa wa Njombe.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,

Akiwa Mkoani humo Mh. Edward Lowassa amewataka Wananchi wa mkoa huo wasiewe na wasiwasi pindi atakapoingia na madarakani na nchi itakua katika hali ya usalama na ataendesha mchakamchaka wa maendeleo kwa kasi kubwa.

Mh. Lowassa ameongeza kuwa ilani ya Ukawa iliyotengenezwa ndio dawa ya matatizo ya Watanzania ambayo ndani ya miaka mitano itaweza kubadilisha taifa pamoja hali ya uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Nae mgombea Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA Mh. Juma Haji Duni amesema Serikali ya Umoja wao utaimarisha sekta ya kilimo cha Korosho katika mikoa ya Pwani na kuondoa Mfumo wa Stakbadhi ghalani na kuboresha bei ya Mazao ili kumuinua Mkulima.

Mh. Juma Haji Duni amesema kuwa mfumo huo unamkandamiza mkulima na kufanya kuendelea kuwa Masikini kutokana na Wakulima kulipwa hela kiasi kidogo na kiasi kikubwa kubaki kwa Serikali na kushindwa kuandaa mashamba yao kwa Wakati.

Mzee Duni amesema kuwa Serikali kuwakopa wakulima na kuchelewesha kuwalipa kwa Wakati ni kuwaonea na kuzidi kuwadidmiza katika lindi la Umasikini hivyo serikali ya UKAWA italiondoa suala hilo na kuleta ahuheni kwa Wakulima na kuinua uchumi wa wa nchi.