Jumanne , 14th Oct , 2025

Nchi hiyo ya Kusini-mashariki mwa Asia ilisema siku ya Ijumaa kuwa imewanyima visa wachezaji wa mazoezi ya viungo wa Israel huku kukiwa na hasira juu ya vita vya mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza.

Shirikisho la Mazoezi ya viungo la Israel limesema juzi Jumapili kwamba linakata rufaa uamuzi wa Indonesia wa kuwazuia wanariadha wake kushiriki katika mashindano ya dunia, likitaja hatua ya taifa hilo kubwa lenye Waislamu wengi kuwa ya kuchukiza.

Nchi hiyo ya Kusini-mashariki mwa Asia ilisema siku ya Ijumaa kuwa imewanyima visa wachezaji wa mazoezi ya viungo wa Israel huku kukiwa na hasira juu ya vita vya mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza.

Timu ya Israeli ilikuwa imeratibiwa kushiriki katika Mashindano ya Ulimwengu ya Mazoezi ya Kisanaa kuanzia Oktoba 19 hadi 25 huko Jakarta.

Waziri Mwandamizi wa Masuala ya Kisheria wa Indonesia, Yusril Ihza Mahendra alisema uamuzi huo ulitokana na pingamizi kutoka kwa makundi kama vile Baraza la Viongozi wa Kiislamu na serikali ya mtaa ya Jakarta.

Aliongeza kuwa hatua hiyo inaendana na sera ya muda mrefu ya Indonesia ya kutokuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Israel hadi itambue uhuru na mamlaka kamili ya Taifa la Palestina.