Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha roli na basi, iliyotokea huko katika eneo la Mnada wa Tinde wilayani Shinyanga, mkoani hapa
Kwa upande wake, mmoja wa majeruhi, Robert Daudi, amesema alikuwa akisafiri na watoto wake watatu, na kwamba waliposikia kishindo kik#ubwa ndipo waligundua kuwa wamepata ajali, hata hivyo watoto wake wako salama. 5), aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili RAE 849 N kutoka nchini Rwanda, ambaye alikuwa amebeba shehena ya mchele.
Ajali hiyo ilihusisha basi la Kampuni ya Kisire lenye namba za usajili T 229 EEL, lililokuwa likisafiri kutoka Kahama kwenda Mwanza.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, akizungumza wakati akiwa eneo la tukio amesema kuwa basi hilo lilikuwa likiendeshwa kwa mwendokasi, na lilipofika katika mnada wa Tinde liligonga toroli la matikiti kabla ya kugongana uso kwa uso na roli hilo.
Magomi amesema basi hilo lilikuwa na jumla ya abiria 42, ambapo 12 walijeruhiwa, kati yao, watano hali zao ni mbaya na wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Mwawaza, huku wengine saba wakipatiwa matibabu katika Zahanati ya Tinde.
“Chanzo cha ajali hii ni uzembe wa dereva wa basi la Kisire ambaye hakuchukua tahadhari. Baada ya ajali kutokea alikimbia, na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka ili achukuliwe hatua za kisheria,” amesema Kamanda Magomi.
Kwa upande w ake, mmoja wa majeruhi, Robert Daudi, amesema alikuwa akisafiri na watoto wake watatu, na kwamba waliposikia kishindo kikubwa ndipo waligundua kuwa wamepata ajali, hata hivyo watoto wake wako salama.Kwa upande wake, mmoja wa majeruhi, Robert Daudi, amesema alikuwa akisafiri na watoto wake watatu, na kwamba waliposikia kishindo kikubwa ndipo waligundua kuwa wamepata ajali, hata hivyo watoto wake wako salama.





