Jumatano , 19th Aug , 2015

Serikali mkoani‭ ‬Iringa‭ ‬imefanikiwa kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya,‭ ‬kilimo na barabara katika kipindi cha mwaka‭ ‬2010‭ ‬hadi‭ ‬2015.

Mkuu wa mkoa wa iringa Bibi Amina Masenza.

Serikali mkoani‭ ‬Iringa‭ ‬imefanikiwa kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya,‭ ‬kilimo na barabara katika kipindi cha mwaka‭ ‬2010‭ ‬hadi‭ ‬2015.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza amesema‭ ‬hayo leo wakati anawasilisha‭ ‬taarifa ya‭ ‬utekelezaji‭ ‬wa Ilani ya‭ ‬Uchaguzi ya‭ ‬Chama cha Mapinduzi‭ (‬CCM‭) ‬ya mwaka‭ ‬2010.

Bibi Masenza amesema‭ ‬sekta binafsi,‭ ‬serikali kuu,‭ ‬serikali za‭ ‬mitaa,‭ ‬wananchi na wadau wameshiriki katika shughuli za maendeleo.

Aidha,‭ ‬mkuu wa mkoa‭ ‬wa Iringa amesema‭ ‬mkoa wa Iringa umekabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi.

Hata hivyo,‭ ‬mkuu wa mkoa wa Iringa Bibi Masenza‭ ‬amesema‭ ‬serikali inatarajia kuongeza‭ ‬ukusanyaji‭ ‬wa‭ ‬kodi ili‭ ‬kutatua‭ ‬changamoto‭ ‬ambazo zinaukabili mkoa huo.‭