Alhamisi , 6th Aug , 2020

Watanzania wote wameombwa kutumia mfumo mpya uluioanzishwa wa huduma kwa wateja ili kuepuka kusafiri safari ndefu kwenda makao makuu ya TAMISEMI kwa ajili ya kupata huduma.

Waziri wa Ofisi ya  Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo

Hayo yamesemwa leo Agosti 6, 2020 mkoani Dodoma na Waziri wa Ofisi ya  Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo, alipokuwa anaongea na waandishi wa habari juu ya wizara hiyo kuanzisha kituo kipya  cha huduma kwa wateja ambacho kitarahisisha wizara hiyo kutoa huduma zake na kuhakikisha zinafika katika jamii kwa haraka.

“Niwaombe watanzania wote TAMISEMI imekuja na mfumo wa Huduma kwa wateja, tumieni mfumo huu wa huduma kwa wateja ambao TAMISEMIM imeamua kuwaletea kwaajili ya kupunguza suala zima la watu kusafiri kujua makao makuu Dododma kupata huduma”

Aidha Mhe.Jafo amewaomba wafanyakazi watakao kuwa wanahudumia wateja kufanya kazi yao kwa ufanisi bila kuchoka kwani wao ndio kioo cha wizara hiyo huku wakizingatia kutoa huduma bora kwa mteja  ili waweze kupata mrejesho mzuri.

“Niwaombe kikosi kazi nyinyi ndio sura yetu ya TAMISEMI,nyinyi mna kazi kubwa sana yakufanya kuliko mtu yeyote, Muonekano wa kwanza una umuhimu, muonekano wetu wa kwanza tukionekana vibaya tutaonekana vibaya, naomba mkajitume sana sana msichoke katika kazi yenu lakini majibu yenu yanatakiwa yawe sahihi bila kuleta ubabaishaji wowote”, ameeleza.

Pia ameeleza kuwa, “Kwa Kituo hiki cha Huduma kwa wateja TAMISEMI, tutaweza kuwasikiliza watu wetu kwa urahisi na ukaribu zaidi lakini tutaongeza kasi kwenye kufanya kazi na tutaweza kupata mrejesho kutoka kwa wateja wetu katika utoaji wa huduma”.