Jumanne , 13th Mar , 2018

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amefuta ada kwa nyaraka mbalimbali za kimahakama na kutaka kutolewa bure kuanzia Mahakama Kuu mpaka ngazi ya Mahakama ya Mwanzo.

Jaji Prof. Juma amewaelekeza Manaibu Wasajili wa Mahakimu Wafawidhi kuhakikisha kuwa maelekezo hayo yanatekelezwa mara mojakwa kuweka mfumo wa kufuatilia utoaji wa nyaraka  hizo kwa wadaiwa  kwa wakati na bila ya malipo yoyote.

Aidha Jaji Mkuu amewataka wananchi kutoa taarifa za ujumbe mfupi kupitia namba ambazo zimebandikwa katika kuta za mahakama endapo wataendelea kudaiwa malipo ili kupata nyaraka hizo za mahakama au iwapo atacheleweshwa kupata maamuzi ndani ya siku 21.