Ijumaa , 11th Sep , 2020

Aliyekuwa Mwanasheria wa kwanza wa Serikali, Jaji Mstaafu Mark Bomani atazikwa siku ya Jumatatu, Septemba 14 katika shamba lake lililopo Goba jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa Mwanasheria wa kwanza wa Serikali, Jaji Mstaafu Mark Boman enzi za uhai wake

Akitoa ratiba hiyo mtoto wa marehemu Bomani, Andrew Bomani amesema kuwa marehemu alichagua kuzikwa eneo hilo na wao kama familia wanafuata maagizo yake.

“Tulitamani kwenda kupeleka msiba nyumbani (Jijini Mwanza), Lakini Baba alisema azikwe hapa Dar es Salaam kwenye shamba lake lililopo Goba “, amesema Andrew ambaye ni mtoto wa marehemu.

Aliyekuwa Msaidizi wa Jaji Mstaafu Bomani, Leonard Lupilya amemuelezea marehemu kuwa alikuwa Mtu mchapakazi na mwenye upendo kwa kila aliyemzunguka.