
Ripoti zinasema wanafunzi wasiopungua wawili walikimbizwa hosptali na gari la wagonjwa sababu ya majeraha mabaya ya moto kwenye tukio lililotokea mapema hii leo. Wengine tisa wanaaminika kuungua moto lakini sio kwa ukubwa.
Ripoti za awali zinaonyesha jaribio hilo lilihusisha bicarbonate ya sodiamu na spiriti za methylated.
Helikopta, wahudumu wa afya na magari ya zimamoto walionekana katika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada wa haraka.
Kaimu Msimamizi wa Magari ya Wagonjwa wa New South Wales Phil Templemen alisema upepo ndio lioathiri majaribio na kupuliza karibu na baadhi ya kemikali ambazo zilitumika.