Jeshi la Polisi lafanya mabadiliko madogo

Jumanne , 14th Mei , 2019

Jeshi la Polisi limefanya mabadiliko madogo ya kiutendaji kwa kuwahamisha baadhi ya maafisa wake na kuwateua wapya.

Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

Katika mabadiliko hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP, Simon Sirro, amemteua aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmed Msangi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, huku nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime.

Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maulid Mabakila amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es salaam.

Akitangaza uteuzi huo, DCP Ahmed Msangi amewashukuru wananchi wa Dar es salaam pamoja na waandishi wa habari ambao amefanya nao kazi kwa ushirikiano katika kufanikisha kazi yake.

Taarifa yote ya mabadiliko iko hapa chini.