Alhamisi , 21st Mar , 2024

Ukatili dhidi ya watoto umeshika kasi jijini Mwanza baada ya mtoto mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa Majengo mapya, Mabatini jijini humo kuunguzwa na maji ya moto mwanamke mmoja jirani akimtuhimumu kumuibia kiasi cha pesa shilingi elfu 16.

Mtoto aliyeunguzwa mikono kwa maji ya moto na mama ambaye ni jirani yake

Wazazi wa mtoto huyo wamesema mtuhumiwa alikamatwa  hata hivo tayari amepewa dhamana, hivyo kuomba serikali ichukue hatua kali za kisheria.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Majengo mapya Raphael Mathias amekemea kitendo hicho na kuwataka wananchi waache kujichukulia sheria mkononi.

Huu ni mwendelezo wa matukio kadhaa ya ukatili dhidi ya watoto Jijini Mwanza ambayo yameripotiwa na EATV hivi karibuni.