JPM aagiza jambo zito kwa vyombo vya ulinzi

Jumapili , 12th Jan , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwashughulikiwa wale wote wanaopotosha na kudharau vyombo hivyo katika kazi yake.

Rais Dkt. John Magufuli

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mjini Unguja Hapo Januari 10, 2020, ambapo amesema ni wajibu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha nchi inakuwa salama na wasikubali kudharauliwa na mtu yoyote.

"Siku hizi kumekuwa na tabia ya hovyo imejitokeza kwa baadhi ya Watanzania wachache. Kila kitu kinachofanywa ni Usalama wa Taifa, mtu akipotea siku mbili hata kama hajapotea yupo kwa mpenzi wake ni Usalama wa Taifa", amesema Rais Magufuli.

"Niviombe vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama likiwemo Jeshi la Polisi ambao huwa mshughulikia wahalifu, msiwaache wahalifu waanze kuchafua vyombo vya Ulinzi na Usalama. Mtu akizungumza amempotea huyu ana ushahidi mshikeni mpaka atoe ushahidi", ameongeza.

Tazama hapa akizungumza zaidi.