Jumanne , 15th Oct , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ameagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini, ibadilishwe na iitwe Halmashauri ya Mtama kwa kile alichokieleza kwamba, watendaji wengi wa Serikali kubaki mjini, kunachelewesha maendeleo kwa wananchi wanaoishi vijijini.

Rais Magufuli akiwa na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Oktoba 15, 2019, wakati akizungumza na wakazi wa Mtama, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Lindi.

''Halmashauri hii haitaitwa tena ya Lindi Vijijini, itaitwa Halmashauri ya Mtama na haya maagizo niliyoyatoa, nitayatoa leo kwa Waziri Jafo wa TAMISEMI ili aweze kuyashughulikia kwa mujibu wa sheria'' amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ametoa siku 15 kwa Halmashauri mbili, ikiwemo Korogwe na Bunda ili kuhakikisha wananzitatua kero alizozitatua leo mkoani Lindi, kabla ya huo muda alioutoa.