JPM amtengua kiongozi anayetuhumiwa kuchukua wake

Jumapili , 28th Jun , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ameagiza kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mtela Mwampamba, ambaye ametengua uteuzi wake hii leo apangiwe kazi nyingine ya chini ambayo atakuwa na uwezo nayo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Juni 28, 2020, baada ya kutengua uteuzi huo kwa madai ya kwamba, amekuwa akifanya mambo ambayo hayaendani na maadili ya kazi yake,ikiwemo tuhuma ya kuchukua wake za watu.

"Hapa kuna tatizo moja la mteule wangu mmoja DAS, ninaambiwa ana mambo ambayo hayaendani na maadili ya kazi yake, zipo tuhuma anachukua hata wake za watu, nilikwishamuonya siku za nyuma nafikiri hakuweza kuonyeka na kwa sababu jukumu langu pia ni kusimamia maadili ya watendaji, ninakuagiza Jafo uongee na Mkuchika kwamba, huyu kazi ya U-DAS nimeitengua leo, mtafutieni kazi ya chini ambayo ana uwezo nayo na asifanye hapa" - Rais Magufuli.

Mara baada ya kauli hiyo Rais Magufuli akamteua muda huo huo, aliyekuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mwanana Msumi kuchukua nafasi hiyo.