Jumamosi , 16th Dec , 2017

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imepongezwa kwa kuonyesha kwa vitendo utekelezaji wa sera ya elimu bure kwa wanafunzi nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwanafunzi Radhia Salumu wa shule ya sekondari Salma Kikwete leo alipohudhuria tamasha la  Coke5Seleket Concert linaloendelea katika Viwanja vya  Leaders Kinondoni Jijini  Dar es Salam, ambapo amesema kwamba ni matumaini yake elimu hiyo (bure) itaendelezwa mpaka vyuoni. 

"Ni vyema watanzania tumpongeze JPM kwa juhudi zake za kutoa elimu bure sio rahisi, naamini hii itafika hadi chuo kikuu " amesema.

Mbali na hayo mmoja wa wanafunzi kutoka shule ya sekondari Kambangwa aliyejulikana kwa jina la Ashura Iddi amesema hakuna njia ya mkato katika kutafuta elimu na kuwashauri wanafunzi wenzake  kutokata tamaa katika kuitafuta elimu ili wajikomboe katika janga la umasikini.

"Naamini katika elimu lazima uwe na uvumilivu ili  uweze kufanikiwa hakuna njia ya mkato katika kutafuta elimu. Sisi tunatakiwa kujiandaa katika maisha yetu ya baadae hivyo tujitahidi katika masomo, "amesema

Wanafunzi kutoka Maeneo Mbali Mbali ya Dar es Salama na maeneo ya jirani wamejitokeza na kujumuika kwa pamoja katika tamasha la Coke5Seleket Concert linaloendelea katika Viwanja vya  Leaders Kinondoni Jijini  Dar es Salama. 

Tamasha la Coke5Seleket Concert  limeandaliwa na Coca Cola ikishirikiana na East Africa LTD likiwa na lengo la kuwakutanisha wanafunzi na kusherehekea kwa pamoja kipindi hiki cha likizo.

Mpaka sasa tamasha hilo linaendelea huku wasanii Mbali Mbali wakiendelea kuishambulia 'Stage'. 

Msanii Rosa Ree akifanya yake jukwaani

Gigy Money akiwa jukwaani