Jumapili , 16th Aug , 2020

Rais Magufuli leo Agosti 16, 2020, ameshiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la Parokia ya Chamwino Ikulu Dodoma.

Rais Magufuli akiwa kanisani.

Akizungumza wakati wa Ibada hiyo Padre Paul Mapalala, amesisitiza suala la kutendeana wema bila kudharauliana na kuwasihi waumini kumuomba Mungu wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili ukafanyike kwa amani na kuchagua viongozi bora.

"Yule unayemdharau ndiyo anaweza kuwa msaada kwako, Sala zake zinakusaidia tunapotendeana vizuri bila kudharauliana heshima inakuwa kubwa, tumuombe Mungu katika kipindi huku tunakoelekea Uchaguzi, tumuombe Mama Bikra Maria msimamizi wa Parokia yetu Maria Immaculata,atuombee kwa Mungu tuweze kuvuka katika kipindi hiki tukaweze kupata viongozi waliobora wapenda amani", amesema Padre Mapalala.