Magufuli asema neema inakuja kwa wafanyakazi

Jumanne , 20th Oct , 2020

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo tarehe 20 Oktoba akiwa Korogwe (Tanga) amewambia mamia kwa maelfu ya waliojitokeza kumsikiliza kuwa kwa miaka mitano ijayo wafanyakazi wataboreshewa maslahi yao na kuongeza kuwa malimbikizo yao

Pichani ni Dkt John Pombe Magufuli, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM.

 yote yanaendelea kushughulikiwa.

Huku akishangiliwa na hadhira hiyo, amezitaja sababu za kutoboresha maslahi ya wafanyakazi kwa miaka mitano iliyopita kuwa ilikuwa ni kuboresha kwanza uchumi wa nchi, kuondoa wafanyakazi hewa, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi ili kuongeza mapato ya nchi.

"Kwasababu uchumi umeimarika, mapato yamekuwa mazuri na miundombinu mingine yote tumemaliza afya, mabarabara na maji  tunaendelea kutengeneza, elimu bure tunaendelea kutoa sasa katika kipindi cha miaka mitano itakuwa kazi pia ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa Tanzania, unaanza uchumi kwanza ndipo utapandisha mishahara, huwezi kupandisha mishahara wakati huna hela ya  kupandisha mishahara" Dkt. John Magufuli

Aidha Magufuli amebainisha kuhusiana suala la serikali kuajairi ''Tumeajiri wafanyakazi zaidi ya 74 elfu katika kipindi cha miaka mitano, walimu zaidi ya 17 elfu, sekta ya afya zaidi ya 14 elfu na wafanyakazi pia katika sekta nyingine''.