Kabendera aombwa

Jumanne , 11th Feb , 2020

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwanadishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera, leo Februari 11, 2020 iliendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo upande wa mashtaka umeomba kukutana na Kabendera kwa mazungumzo binafsi.

Mwandishi wa Habari Erick Kabendera, anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi.

Uamzi huo umefikiwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Janeth Mtega, baada ya Wakili Mkuu wa Serikali Faraja Nchimbi, kuwasilisha ombi hilo kwa lengo la wao kukutana na mshtakiwa na kukamilisha majadiliano ili kumaliza kesi hiyo.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu, ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na utakatishaji wa fedha zaidi ya shilingi milioni 170.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 17, mwaka huu itakapotajwa tena.