Jumatatu , 19th Jan , 2015

Watanzania wametahadharishwa kutowasikiliza wanasiasa wenye nia ya kuvunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwani katika kipindi cha miaka 51 ya Muungano huo, kumekuwa na mafanikio kwa pande zote mbili

Katibu wa NEC itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM,Ndugu Nape Nnauye.

kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Magharibi Unguja, bwana Yusufu Mohamedi Yusufu, wakati akiwakaribisha kuhutubia mkutano wa hadhara, viongozi wa juu wa chama hicho, wanaoendelea na ziara katika visiwa vya unguja na pemba, ambapo amewatahadharisha watanzania kutokubali hadaa za wanasiasa wenye nia ya kuvunja muungano kwa maslahi yao binafsi,.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu wa CCM itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye amemtaka Makamu wa kwanza wa Rais ambaye pia ni katibu Mkuu wa CUF taifa Maalim Seif Sharif Hamad ajiuzulu nafasi hiyo kama hataki Muungano wa Serikali mbili.

Nape amepinga kauli ya katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF aliyodai haina mashiko kufuatia chama cha CUF kudai kuchukua majimbo 18 ya uwakilishi na ubunge katika uchaguzi ujao na kudai kuwa wamejipanga kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo, kauli inayoungwa mkono na katibu mkuu wa chama hicho komredi Abdulrahman Kinana.

Wakihutubia wananchi waliofurika katika uwanja wa Tomondo baadhi ya viongozi wa chama hicho walioambatana na katibu mkuu upande wa Zanzibar wakiwemo wabunge wa bunge la jamuhuri ya mungano wa Tanzania na wawakilishi wa baraza la wawakilishi la serikali ya mapinduzi Zanzibar wamesihi wazanzibar kuipigia kura ya ndiyo katiba iliyopendekezwa muda utakapo wadia.