Alhamisi , 25th Nov , 2021

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amesema kuwa bajeti ya Jiji itakayopitishwa kwa mwezi Desemba, watahakikisha wanapambana kuingiza bajeti ya kununua CCTV camera na taa zitakazofungwa katika soko la Kariakoo ili liwe eneo salama zaidi kwa wafanyabiashara.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 25, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio.

"Lengo letu ni kuifanya Kariakoo watu wafanye kazi saa 24 yaani usiku na mchana,", amesema Meya Kumbilamoto