Kasesela atangaza kupambana na Halima Mdee

Jumatatu , 22nd Jun , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema kuwa tarehe 14, atachukua fomu kwa ajili ya kutia nia ya kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kawe kwa kuwa anayo nguvu kubwa katika jimbo hilo na kumng'oa rasmi Halima Mdee.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na kulia ni Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Hayo ameyabainisha leo Juni 22, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast, ambapo pia ameeleza majukumu ya Mkuu wa Wilaya katika eneo husika, ikiwemo usimamizi wa shughuli zote za Serikali katika Wilaya, pamoja na kuwa msimamizi wa shughuli za ulinzi na usalama.

"Nilishawaambia nina majimbo matatu, hiyo tarehe 14 mtasikia tu nimechukua fomu, maana hapo Kawe nina nguvu kubwa tu, utasikia tu rafiki yangu Mdee ananiambia, Kasesela usije huku, lakini pia na Mchungaji hapa anatakiwa ang'oke sasa tutaangalia tu, mimi nacheza na nyota ya Mungu" amesema Kasesela.