Jumatatu , 25th Oct , 2021

Mkurugenzi wa bar maarufu ya The Cask ya jijini Mwanza, Joe Makanyaga, ambayo imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Oktoba 25, 2021, amesema kuwa ataangalia namna ya kuanza upya na wafanyakazi ambao alikuwa anafanya nao kazi tangu mwanzo.

Moto ukiteketeza bar ya The Cask

Joe amesema kuwa moto huo umegharimu kwa kiasi kikubwa maisha ya wafanyakazi pamoja na yeye kibiashara na kusema kwamba yeye kama mfanyabiashara anatambua uwepo wa hasara za namna hiyo na kwamba huo siyo mwisho wa bar hiyo bali ataanza upya.