Kenya : Magaidi wavamia Shule, wauwa Walimu

Jumatatu , 13th Jan , 2020

Watu wanaodhaniwa kuwa ni magaidi wa kundi la Al - Shabaab, wamewaua watu watatu wanaodaiwa kuwa ni Walimu katika Shule ya Kamuthe Resource Center ya nchini Kenya katika eneo la Garissa.

Tukio hilo limetajwa kutokea alfajiri ya kuamkia leo Januari 13, 2020, baada ya magaidi hao kudaiwa kuvamia Shule hiyo.

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa EATV kutoka nchini Kenya, amesema magaidi hao pia wamezima mawasiliano kwenye Mji huo wa Garissa, kwa kuharibu mnara wa simu wa kampuni ya Safaricom.

Tutaendelea kukuletea taarifa kila wakati kuhusiana tukio hilo.