Kenya yafunga mipaka ya Tanzania ya Somalia

Jumamosi , 16th Mei , 2020

Kenya imethibitisha kuwepo kwa kesi mpya 49 za maambukizi ya Covid-19 na kufanya kuwa na jumla ya kesi 830, huku vifo vikifika 50.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Akihutubia taifa leo Mei 16, 2020 Rais Uhuru Kenyatta ametangaza pia kuongeza siku 21 za lockdown nchi nzima muda wa jioni hadi asubuhi, pamoja na kufunga mipaka ya Tanzania na Somalia kwenye baadhi ya huduma.

''Tunaongeza siku 21 za 'lockdown' nchini lakini mipaka yetu ya Tanzania na Somalia tunaifunga lakini upande wa usafirishaji wa bidhaa tunaachia kwa makubaliano ya madereva kupimwa Covid-19 na kuonyesha vyeti mipakani'', amesema Uhuru.

“Watu wengine watano wamefariki baada ya kuugua corona na kufanya idadi ya waliofariki na corona kufikia 50,  tuna wagonjwa wapya 49 pia na hii inafanya maambukizi ya corona kufikia 830 Kenya, wagonjwa 17 wamepona na kufanya waliopona kufikia 301” - Kenyatta.
 

Msikilize hapo chini akieleza.