Ijumaa , 24th Oct , 2025

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, leo Ijumaa, Oktoba 24, 2025, ametembelea Soko la Darajani lililopo Malindi, Visiwani Zanzibar, ambako amezungumza na

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, leo Ijumaa, Oktoba 24, 2025, ametembelea Soko la Darajani lililopo Malindi, Visiwani Zanzibar, ambako amezungumza na wafanyabiashara na kutoa elimu kuhusu namna sahihi ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Makonda ameendelea na ziara zake katika mikoa mbalimbali nchini akifanya kampeni za uhamasishaji wa wapiga kura kumuunga mkono Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho.

Aidha, mbali na kutoa elimu ya kupiga kura, mgombea huyo amewasihi wananchi kuendelea kuwa watulivu na kuepuka vitendo vyovyote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.