Jumanne , 11th Nov , 2025

Niffer na wenzake 21 wanaosimamiwa na Wakili Peter Kibatala wanakabiliwa na makosa matatu.

Kesi ya uhaini inayomkabili mfanyabiashara Jenifer Jovin na wenzake inaendelea tena leo Novemba 11, 2025 baada ya Novemba 7, 2025 Niffer na wenzake 21 kulifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka hayo yanayowakabili.

Niffer na wenzake 21 wanaosimamiwa na Wakili Peter Kibatala wanakabiliwa na makosa matatu. Kosa la kwanza linalowahusu washtakiwa wote 22 wakidaiwa kula njama ya kutenda kosa au kupanga uhalifu ambao ni uhaini.

Kosa la pili ambalo ni la uhaini linawahusu washtakiwa 21 isipokuwa mshtakiwa mmoja pekee ambaye ni Niffer, ambapo  ambao walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi Mkuu 2025, na kutishia mamlaka na wakatekeleza nia hiyo kwa kufanya vurugu zilisababisha uharibifu wa mali za umma,

Na kosa la tatu la uhaini pia linamuhusu mshtakiwa namba moja pekee ambaye ni Niffer, ambapo alihamasisha watu kuvuruga uchaguzi Mkuu 2025 na kuhamasisha umma kununua barakoa za kuzuia mabomu ya machozi kutoka dukani kwake.

Siku hiyo na Novemba 7, 2025 jumla ya washtakiwa 240 walifikishwa katika mahakama hiyo na kusomewa mashtaka ya kula njama ya kutenda kosa au kupanga uhalifu la uhaini na uhaini wenyewe.