Jumatano , 2nd Nov , 2016

Mahakama ya Afrika Kusini imesikiliza shauri lililowasilishwa na Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, akitaka kuzuiwa kwa uchapishaji wa ripoti ya uchunguzi wa uhusiano wake na familia tajiri ya wafanyabiashara wa kihindi.

Jacob Zuma

 

Rais Zuma katika shauri hilo anadai kwamba hakupewa muda wa kutosha kujibu maswali aliyoulizwa na msimamizi wa maslahi ya umma Thuli Madonsela, wakati wa uchunguzi huo ulipachikwa jina la ''Kukamatwa kwa Dola'' na familia ya Gupta.

Uchunguzi huo ulilenga kubainisha shutuma kwamba Zuma aliiruhusu familia hiyo kuwa na ushawishi wa kisiasa kupindukia, ikiwemo kauli kuhusu uteuzi wa mawaziri.

Vyama vinne vya upinzani vinapinga shauri hilo katika mahakama kuu ya mjini Pretoria.