Jumapili , 8th Jun , 2025

Mmarekani Coco Gauff ameshinda taji lake la kwanza la French Open baada ya kumshinda nyota namba moja Duniani kwa upande wa wanawake Aryna Sabalenka kwa seti 6-7,6-2 na 6-4

Coco Gauff

Ushindi huo alioupata leo  ni ushindi wa pili wa Grand Slam kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21  Grand Slam nyingine aliyonayo mwanadada huyo ni  US Open aliyoshinda 2023 kwa kumshinda Sabalenka mwenye umri wa miaka 27

Kwa upande wa wanaume fainali yao itapigwa kesho ikimkutanisha Jannik Sinner dhidi ya Carlos Alcaraz